Karate
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Karate (pia kareti, kutoka Kijapani: 空手) ni aina ya michezo ya mapigano kutoka nchini Japani.[1] Ilianzishwa kwenye kisiwa cha Okinawa ikaenea Japani kwenye mwanzo wa karne ya 20 na kusambaa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[2]






Karate inatumia kama silaha za mapigano pande zote za mwili kama vile mkono, ngumi, kisugudi au mguu.
Mafunzo ya karate huwa na ngazi tatu:
- kihon inahusu misingi
- kata ni namna ya kutumia misingi hiyo
- kumite ni matumizi yake katika mapigano
Kati ya michezo ya mapigano kama mchezo wa ngumi au kupiga mwereka karate inaweka mkazo kwa nguvu ya kiroho sawa na nguvu ya mwili.
Karate imefahamika duniani zaidi kutoka filamu za karate kuanzia miaka ya 1960.
Mwalimu wa karate kwa Kijapani huitwa "sensei" (kwa Kiingereza "master").
Remove ads
Nguo za Karate
Wakati wa kucheza karate watu huvaa nguo za pekee zinazoitwa karategi ambazo ni suruali na jaketi nyeupe. Juu ya jaketi huwa na mkanda wenye rangi fulani. Rangi inaonyesha cheo ambacho mtu amefikia katika ujuzi wa karate. mkanda mweusi huonyesha cheo cha juu.
Karate katika Mchezo ya Olimpiki
Karate itachezwa kwa mara ya kwanza katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2021 mjini Tokyo.[3]
Viungo vya Nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads