Kibondo (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa maana nyingine ya jina hili angalia Kibondo (maana)

Kibondo ni mji mdogo na makao makuu ya wilaya ya Kibondo katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania. Mji uko kilomita 270 kaskazini kwa Kigoma, karibu na mpaka wa Burundi.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,268 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 39,300 waishio humo.[2]
Wenyeji wa Kibondo ni hasa Waha.
Mwaka 1993 wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi wakimbizi wengi walifika Kibondo na kambi tatu zilijengwa kando ya mji wa Kibondo. Kambi hizo zilikuwa na Warundi zaidi ya 25,000 waliokuwa zaidi ya robo ya wakimbizi wote kutoka Burundi nchini Tanzania. Kambi hizo ni Nduta, Kanembwa na Mtendeli. Zililongeza kasi ya biashara mjini lakini pia zilisababisha matatizo mbalimbali, hasa ya kiusalama na ya kimazingira.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads