Kibwirosagi
Ndege wa jenasi mbalimbali za familia Cisticolidae From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Vibwirosagi ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na wana rangi kali zaidi: nyekundu, kijani, kahawia na/au kijivu mgongoni na njano, nyekundu, marungi, hudhurungi na/au kijivu chini. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulijenga tago lenye kuba ya manyasi, majani na/au vigoga katika kichaka, mmea au dege la watoto. Jike huyataga mayai 1-4.
Remove ads
Spishi
- Bathmocercus cerviniventris, Kibwirosagi Tumbo-hudhurungi (Black-Headed Rufous Warbler)
- Bathmocercus rufus, Kibwirosagi Uso-mweusi (Black-Faced Rufous Warbler)
- Eminia lepida, Kibwirosagi Utosi-kijivu (Grey-capped Warbler)
- Euryptila subcinnamomea, Kibwirosagi Kidari-marungi (Kopje au Cinnamon-breasted Warbler)
- Hypergerus atriceps, Kibwirosagi Kichwa-cheusi (Oriole Warbler)
- Incana incana, Kibwirosagi wa Sokotra (Socotra Warbler)
- Malcorus pectoralis, Kibwirosagi Masikio-mekundu (Rufous-eared Warbler)
- Scepomycter rubehoensis, Kibwirosagi wa Rubeho (Rubeho Warbler)
- Scepomycter winifredae, Kibwirosagi wa Uluguru (Winifred's au Mrs. Moreau's Warbler)
Remove ads
Picha
- Kibwirosagi uso-mweusi
- Kibwirosagi utosi-kijivu
- Kibwirosagi kidari-marungi
- Kibwirosagi wa Sokotra
- Kibwirosagi masikio-mekundu
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads