Kifafa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kifafa
Remove ads

Kifafa (kwa Kiingereza Epilepsyis, kutoka kitenzi cha Kigiriki ἐεπιλαμβάνειν, eepilambanein, kuteka au kutesa[1]) ni kundi la maradhi ya neva yanayofanana kwa dalili za matukio ya kupatwa,[2] ambayo yanaweza kudumu muda mfupi sana karibu bila kugundulika hadi muda mrefu wa kutikisika kwa nguvu mwili mzima.[3] Matukio hayo yanaelekea kurudiarudia bila sababu inayoeleweka kwa kila tukio[2] wakati matukio ya namna hiyo yenye sababu inayoeleweka si ya kifafa kweli.

Picha za video kuhusu matukio ya kifafa.
Thumb
Majeraha ulimini yaliyosababishwa na anguko.
Remove ads

Visababishi

Sababu ya kesi nyingi haijulikani, ingawa baadhi ya watu wanapatwa na kifafa kutokana na jeraha la ubongo, kiharusi, saratani ya ubongo na matumizi mabaya ya dawa. Mabadiliko ya DNA yanahusiana moja kwa moja na asilimia ndogo za kesi zote.[4]

Matukio ya kifafa yanatokana na utendaji mkubwa mno wa neva za ubongo.[5]

Ili kusema ni kifafa, daktari anapaswa kwanza kutambua hakuna sababu zinazoeleweka za dalili kama hizo, kwa mfano kuzimia.[4] Mara nyingi kifafa kinaweza kuthibitishwa na electroencephalogram (EEG).[4]

Remove ads

Tiba

Katika 70% za matukio inawezekana kuyadhibiti.[6] Isipowezekana tiba, pengine upasuaji, uchocheaji wa neva na mabadiliko ya ulaji vinatumika. Si kila mara kifafa kinadumu maisha yote: kuna watu wanaopata nafuu kiasi cha kutohitaji tena dawa.

Uenezi

Karibu 1% ya watu wote duniani (milioni 65) wana kifafa,[7] na karibu 80% za kesi zinatokea katika nchi zinazoendelea.[3]

Mwaka 2013 vilitokea vifo 116,000, ambavyo ni vingi kuliko vile 112,000 vya mwaka 1990.[8]

Kifafa kinazidi kutokea kadiri watu wanavyokua.[9][10][11][12]

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads