Kipimo cha mjao
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kipimo cha mjao (pia: kipimo cha ujazo, kizio cha ujazo) ni namna ya kutaja mjao au kiasi cha kiowevu (kwa mfano maji), gesi au vitu vya kumwaga kama unga au nafaka.
Ni pia kipimo cha kutaja nafasi ndani ya chombo, jengo au gimba la kijiometria kwa jumla.
Vipimo vya SI
Kipimo sanifu cha kimataifa cha mjao ni mita ya ujazo (alama m³) inayoweza kugawiwa kwa vizio vidogo kama vile desimita ya ujazo au sentimita ya ujazo; kwa kutaja mjao wa magimba makubwa ya maji kama vile ziwa au bahari uwingi wake ni kawaida kutumia uwingi wake yaani kilomita ya ujazo.
Kipimo cha kawaida cha kutaja viowevu kama maji, mafuta au kinywaji ni lita inayolingana na desimita ya ujazo.
Remove ads
Vipimo vya kimila
Kabla ya kuundwa kwa vipimo vya SI kulikuwa na vipimo mbalimbali vya mjao vilivyo tofauti kati ya nchi na nchi.
Vipimo vya Kiingereza
Hadi leo vipimo vya kiutamaduni vya Uingereza bado vinatumiwa katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza kama Marekani, Ufalme wa Maungano au Australia na hapo na pale kati ya watu wa nchi zilizokuwa koloni ya Uingereza. Ilhali vipimo vilisanifishwa katika Milki ya Uingereza wakati wa karne ya 19 baada ya Marekani kupata uhuru vipimo viko tofauti kidogo pande zote mbili. Mifumo hii miwli inajulikana kama "imperial units" (Uingereza) na "US customary measurement" (Marekani).
Vipimo vya Uswahilini
Waswahili wa kale kabla ya enzi ya ukoloni walikuwa na mfumo wa vipimo vyao, pia kwa mjao.
Katika biashara walipima hasa mjao wa nafaka. Kipimo cha kimsingi kilikuwa pishi, Pishi 1 iligawiwa kwa visaga 2 au vibaba 4.
Pishi 12 zilikuwa fara 1. Fara 5 au pishi 60 ziliitwa jizla 1, iliyoitwa pia mzo.[1]
Pishi ililingana takriban na lita 2.5 - 3 lakini jinsi ilivyo katika mazingira ya kimila vipimo vilitofautiana kati ya mji na mji au soko na soko.[2]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads