Kisiwa cha Wake
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kisiwa cha Wake ni atoli (aina ya kisiwa) katika Bahari ya Pasifiki, karibu na funguvisiwa la Hawaii. Inasimamiwa na Jeshi la Marekani. Ni eneo la ng'ambo la Marekani, ikihesabiwa kati ya Visiwa Vidogo vya Nje vya Marekani.

Kuanzia Desemba 1941 hadi Agosti 1945 atoli hiyo ilivamiwa na Milki ya Japani.
Jiografia
Jinsi ilivyo na atoli nyingi, umbo la kisiwa ni takriban la duara; ukanda wa nchi kavu ni kama vipande kadhaa kwa hiyo tunaweza kusema atoli yote inafanywa na visiwa vitatu ambavyo kwa jumla huwa na eneo la hektari 737.06.

Kisiwa cha Wake kinahesabiwa kazi ya Visiwa vilivyo mbali kabisa na bara au na kisiwa chochote kingine. Visiwa vilivyo karibu ni Atoli ya Bohak (umbali km 560, hakuna watu) na Atoli ya Utirik (km 953, kuna watu) kwenye Visiwa vya Marshall kwa upande wa kusini-magharibi.
Wake iko km 2,416 upande wa mashariki wa Guam, km 3,698 upande wa magharibi wa Honolulu na km 3,204 upande wa kusini-mashariki wa Tokyo.
Remove ads
Wakazi
Hakuna wakazi wa kudumu kwenye Kisiwa cha Wake, kwa hiyo hakuna shule ya watoto. Takriban watu 100 wanaishi huko wakati wowote. Wengi wao ni wakandarasi wanaotunza barabara, uwanja wa ndege na miundombinu mingine. [1]
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads