Kitabu cha Baruku
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kitabu cha Baruku ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Uandishi
Kadiri ya utangulizi wake (Bar 1:1-14), kiliandikwa na Baruku, karani wa nabii Yeremia, wakati wa uhamisho wa Wayahudi huko Babuloni katika karne ya 6 K.K..
Hata hivyo wataalamu wanaona kiliandikwa katika karne ya 2 K.K. moja kwa moja katika lugha ya Kigiriki, isipokuwa labda sehemu ya pili inatokana na andiko asili la Kiebrania.
Mazingira
Kitabu kinatuingiza katika Uyahudi wa mtawanyiko na kutuonyesha jinsi maisha maadilifu ya kidini yalivyodumishwa kwa kuhusiana na Yerusalemu, kwa kudumisha sala na kushika Torati.
Ufafanuzi
Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads