Deuterokanoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Vitabu vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha[1]) ni maandiko yanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo[2].
Vitabu hivyo viliandikwa miaka 300 - 50 KK[3][4][5].
Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe[6].
Remove ads
Vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale
Katika Biblia zinazotolewa na Kanisa Katoliki ni vitabu saba vifuatavyo (pamoja na sehemu za vitabu vya Kitabu cha Esta na Kitabu cha Danieli):
- Tobiti
- Yudith
- Kitabu cha Wamakabayo I
- Kitabu cha Wamakabayo II
- Hekima
- Yoshua bin Sira
- Kitabu cha Baruk
Baadhi ya Waorthodoksi wana vitabu vingine pia kama vile Kitabu cha kwanza cha Ezra (Ezra ya Kiebrania huhesabiwa kama Ezra 2), Kitabu cha tatu cha Wamakabayo na Zaburi ya 151; kama nyongeza Kitabu cha nne cha Wamakabayo; Ufunuo wa Ezra na hata vingine.
Vitabu hivyo vyote ama havikuandikwa (Bar, 2 Mak, Hek) ama havikupatikana mapema kwa lugha ya Kiebrania (asili kwa Sir, Judt, 1Mak) wala ya Kiaramu (asili kwa Tob), bali kwa Kigiriki tu.
Remove ads
Historia ya orodha ya vitabu vya deuterokanoni
Hadi karne ya 1 KK orodha ya vitabu vya Biblia ya Kiebrania ilikuwa haijaamuliwa, ingawa ilikuwa wazi ya kwamba vitabu vya Torati ni maandiko matakatifu kamili; katika suala la vitabu vingine Wayahudi bado walitofautiana, k.mf. Masadukayo walikataa hata vile vya Manabii vilivyokubaliwa na Mafarisayo.
Sehemu kubwa ya Wayahudi nje ya Israeli na Mesopotamia walitumia toleo la Kigiriki lililoitwa Septuaginta ambalo lilitafsiriwa na wataalamu Wayahudi huko Misri katika karne ya 2 na ya 3 KK.
Kabla ya kukamilika kwa orodha ya vitabu vya Agano Jipya Septuaginta ilikuwa ndiyo Biblia ya Wakristo wa kwanza (ambao wengi wao hawakujua Kiebrania)[7][8].
Baada ya maangamizi ya Hekalu la Yerusalemu (70) na hasa katika karne ya 2 wataalamu Wayahudi, walipopatana juu ya mapokeo yao ili kujiimarisha dhidi ya Ukristo na ustaarabu wa kigeni, waliamua kutovikubali kama sehemu za Tanakh vitabu visivyopatikana kwa lugha ya Kiebrania.
Wakristo hawakufuata maazimio hayo ya Wayahudi, hivyo mwishoni mwa karne ya 2 Wakristo magharibi mwa Mediteranea walianza kutafsiri Septuaginta kwa Kilatini kilichokuwa lugha kuu kwao.
Remove ads
Matamko ya Kanisa Katoliki
Vitabu vya Deuterokanoni vilihesabiwa rasmi kuwa sehemu ya Biblia hasa kuanzia Hati ya Damasi au De explanatione fidei, iliyotolewa na Papa Damasus I mwaka 382 [9].
Tafsiri ya Kilatini ya Hieronimo iliyoitwa Vulgata ilipata kuwa toleo muhimu katika Kanisa Katoliki. Hieronimo mwenyewe alipotafsiri Biblia upya katika Kilatini alisema vitabu vya Septuaginta kama Hekima, Yoshua bin Sira, Yudith na Tobiti havistahili kuwemo katika Biblia[10][11] lakini alivitafsiri ndani ya Vulgata kufuatana na maelekezo wa Papa Damaso I aliyemuagiza kazi [12]
Orodha hiyo ya Papa Damaso I ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo[13][14][15] kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa tatu wa Karthago (397) na Mtaguso wa nne wa Karthago (419)[16].
Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Esuperi wa Toulouse (405)[17].
Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442)[18] na Mtaguso wa Trento (1546)[19] ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki.
Misimamo ya Waprotestanti
Wakati wa Matengenezo ya kiprotestanti katika karne ya 16 Martin Luther na wengineo walishika msimamo mkali kuhusu kanuni ya Biblia akafuata azimio la Wayahudi na shauri la Hieronimo kuhusu vitabu hivyo.
Pamoja na hivyo waliweza kuweka pembeni hata baadhi ya vitabu vya Agano Jipya ambavyo zamani ulitokea wasiwasi juu yake na kwa sababu hiyo pengine vinaitwa pia deuterokanoni[20]:
- Waraka kwa Waebrania,
- Waraka wa Yakobo
- Waraka wa pili wa Petro
- Waraka wa pili wa Yohane
- Waraka wa tatu wa Yohane
- Waraka wa Yuda
- Ufunuo wa Yohane
Baada ya kifo cha Martin Luther, Waprotestanti kwa jumla walikubali tena vitabu vyote vya Agano Jipya[21] na kurudisha umoja katika jambo hilo la msingi kwa Ukristo.
Remove ads
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads