Kiwango cha vifo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kiwango cha vifo (kwa Kiingereza: mortality rate) ni kipimo. Kinataja idadi ya vifo katika kundi fulani la watu katika kipindi maalum.

Mara nyingi hutajwa kama idadi ya vifo katika kundi la watu 1,000 kwa mwaka. Kiwango cha vifo 9 kwa 1,000 kinamaanisha kuna watu 9 waliofariki katika jumla ya watu 1,000 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kiwango cha vifo duniani

Jumla ya kiwango cha vifo hufafanuliwa kuwa "kiwango cha vifo kutokana na sababu zote za vifo ndani ya umma fulani" kwenye kipindi fulani, ikitajwa kama idadi ya vifo kwa watu 1,000 au 100,000.

Kwa mfano, jumla ya umma katika Marekani ilikuwa 290,810,000 kwenye mwaka 2003. Katika mwaka ule vilitokea vifo 2,419,900 kwa jumla. Hii inaleta kiwango cha vifo cha 832 kwa 100,000.[1]

Kwa mwaka 2020 kuna kadirio kuwa kiwango cha vifo nchini huko kitakuwa 8.3 kwa 1,000, na duniani kote kitakuwa 7.7 kwa 1,000.[2]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads