Klodolfi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Klodolfi

Klodolfi (pia: Chlodulf, Clodulphe, Clodould, Clou, Cloud; 605 - 697 hivi) alikuwa askofu wa 30 wa Metz (leo nchini Ufaransa) kwa miaka 40 hivi hadi kufikia umri wa miaka 91[1].

Thumb
Mt. Klodolfi na mke wake, Maria.

Baba yake, Arnulfo wa Metz, alitangulia kuwa askofu wa huko, baada ya kuachana na mke wake, Doda, ili yeye aingie upadri na mke umonaki. Kama baba yake, alikuwa pia mshauri wa mfalme wa Austrasia.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Juni[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.