Krispina
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Krispina (Taoura, leo nchini Algeria, karne ya 3 - Tébessa, Numidia, leo nchini Algeria, 5 Desemba 304) alikuwa mwanamke Mkristo aliyeuawa kwa kukatwa kichwa kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya makaisari Dioklesyano na Maximian kwa sababu alikataa kutoa sadaka kwa miungu [1].

Habari za huyo mama wa familia tajiri zinasimuliwa katika hati za mateso yake zilizoandikwa muda si mrefu baada ya tukio na katika hotuba za Augustino wa Hippo[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Filamu
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads