Loyal to the Game

From Wikipedia, the free encyclopedia

Loyal to the Game
Remove ads

Loyal to the Game ni jina la kutaja albamu ya nne kutolewa baada ya kifo cha hayati Tupac Shakur. Albamu ina maremixi kadhaa ambayo awali hayakutolewa na Tupac Shakur kabla ya kifo cha mnamo mwaka wa 1996. Albamu ilitolewa nchini Marekani mnamo tar. 14 Desemba 2004 (12 Desemba nchini Uingereza), Loyal to the Game ilitayarishwa na Eminem.

Ukweli wa haraka Studio album ya 2Pac, Imetolewa ...

Kwa mujibu wa mahojiano yake na MTV, Eminem alivutiwa sana maisha ya Tupac na kazi zake na hivyo kumwandikia barua mama'ke Tupac, Afeni Shakur, akimwomba amruhusu kutayarisha albamu hii. Shakur amekubali, amempa Eminem haki za kuendelea kutayarisha albamu.[1] Albamu imetoa vibao vikali viwili - "Thugs Get Lonely Too" na "Ghetto Gospel".[2]

Eminem ametoa maujanja tofauti kadhaa wakati wa matayarisho ya albamu hii, amebadilisha hatua na uzito wa sauti ya Tupac ili iweze kwenda sawa na biti alizotayarisha.[3] Pia kumekuwa na matumizi mengi ya kukata na kubandika sauti ili kutengeneza maneno mapya yafofuatana na mwenendo wa utamaduni wa rap ya kisasa.

Ilifika kilele cha nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 ikiwa na mauzo zaidi ya nakala 330,000 katika wiki yake ya kwanza. Halafu baadaye ilitunukiwa Platinum nchini Marekani na Dhahabu huko nchini Uingereza.[4]

Remove ads

Orodha ya nyimbo

Maelezo zaidi #, Jina ...
Remove ads

Nafasi za chati za albamu

Mwaka Albamu Chati
Billboard 200 Top R&B/Hip Hop Albums Top Rap Albums Canadian Albums Chart
2004 Loyal To The Game #1 #1 #1 #7

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads