Luteti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Luteti
Remove ads

Luteti (lutetium) ni elementi ya kimetali yenye alama Lu na namba atomia 71. Rangi yake ni nyeupe-kifedha.


Ukweli wa haraka

Katika orodha ya elementi imepangwa katika kundi la metali za mpito na kati ya lanthanidi. Tabia zake hulingana na lanthanidi kwa jumla.

Iligunduliwa mwaka 1907 na wanakemia mbalimbali; ilhali Mfaransa Georges Urbain alikuwa wa kwanza kutoa taarifa zake alipewa haki ya kuchagua jina akateua Luteti kufuatana na Lutetia, jina la kale la Paris.

Ilhali ni metali haba ambayo ni vigumu kuisafisha, tena kwa gharama kubwa, hakuna matumizi mengi ya kibiashara. Inatumika kama kichocheo katika uharibikaji kijoto wa mafuta asilia na michakato mingine ya kikemia.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luteti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads