Majengo (Mbeya mjini)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa maana nyingine za jina hili angalia hapa
Majengo ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 2,958 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,314 [2] walioishi humo.
Msimbo wa posta ni 53110.
Remove ads
Historia
Majengo ni kati ya sehemu za kale kabisa za mji wa Mbeya. Mbeya ilipoanzishwa na Waingereza mnamo mwaka 1927 ilipangwa kufuatana na kawaida ya miji wa kikoloni ya Afrika ya Mashariki kuwa na sehemu tatu[3]:
- Uzunguni kama sehemu ya nyumba za Wazungu na kando lake ofisi za serikali (District Officer, polisi, mahakama)
- Uhindini kama mtaa wa biashara iliyokuwa hasa mkononi mwa wafanyabiashara wenye asili ya Uhindi ya Kiingereza na
- Majengo kama sehemu kwa wafanyakazi Waafrika na familia zao.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads