Malabo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Malabo
Remove ads

Malabo ni mji mkuu wa Guinea ya Ikweta wenye wakazi 155,963 (2005). Uko mwambaoni mwa Atlantiki kwenye pwani ya kaskazini ya kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Po).

Ukweli wa haraka Nchi, - Wakazi kwa ujumla ...
Thumb
Mahali pa Malabo mkoani Bioko Norte.
Thumb
Sehemu ya Mji wa Malabo.
Remove ads

Historia

Mji ulianzishwa kwa jina la Port Clarence mwaka 1827 na Waingereza waliokuwa wamekodi kisiwa cha Fernado Po kutoka kwa Wahispania. Uingereza ulitumia kisiwa kama kituo cha jeshi la uanamaji lilizozunguka Atlantiki kwa shabaha ya kukomesha biashara ya watumwa. Waingereza walipeleka huko watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara ya watumwa. Mwaka 1843 Waingereza walihamisha kituo chao cha kijeshi kwenda Sierra Leone na sehemu ya watumwa wa zamani waliopewa uhuru wao walibaki, wengine wakafuatana na Waingereza kwenda Sierra Leone.

Wahispania walirudi polepole wakabadilisha jina la mji kuwa Santa Isabel.

Tangu uhuru wa Guinea ya Ikweta mwaka 1968 Santa Isabel ikawa mji mkuu. Wakati wa udikteta wa rais Francisco Macías Nguema jina lilibadilishwa kuwa Malabo. Idadi ya wakazi ilipungua sana kutokana na utawala wa kidikteta, wengi walikimbia kama wanachi kwa ujumla. Tangu mwisho wa Macias Nguema idadi imeongezeka tena lakini bado dalili ya uharibifu uliotokea zinaonekana.

Pamoja na hasara hizo Malabo ni kitovu cha kiuchumi cha nchi. Mazao ya kakao, kahawa na mbao yanapelekwa huko kwa meli na kuuzwa nje.

Remove ads

Tanbihi

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malabo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads