Mangosuthu Buthelezi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mangosuthu Buthelezi
Remove ads

Inkosi Mangosuthu ("Gatsha") Ashpenaz Nathan Buthelezi (27 Agosti 1928 - 9 Septemba 2023[1]) alikuwa kiongozi wa Wazulu nchini Afrika Kusini, na vilevile kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) ambacho kiliundwa mwaka 1975.

Thumb
Mangosuthu Buthelezi (1983)

Wasifu

Maisha ya awali

Mangosuthu alizaliwa mnamo 27 Agosti 1928, mjini Mahlabathini, KwaZulu-Natal, na Chief Mathole Buthelezi na binti wa mfalme Magogo kaDinizulu, ambaye ni dada wa mfalme Solomon kaDinuzulu. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Impumalanga iliyoko Mahashini, Nongoma, tangu mwaka 1933 hadi mwaka 1943, kisha katika chuo kimoja kiitwacho Adams College, kilichopo Amanzimtoti, tangu mwaka 1944 hadi 1947.

Baadaye akaelekea katika Chuo Kikuu cha Fort Hare kuanzia mwaka 1948 hadi 1950, ambapo ndipo alipojiunga na chama cha African National Congress Youth League na kuanza kupata mawasiliano na Robert Mugabe na Robert Sobukwe. Mangosuthu alifukuzwa chuoni baada ya wanafunzi kuleta mgomo. Kisha alikuja kumalizia digrii yake katika Chuo Kikuu cha Natal.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads