Mankala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mankala ni jina la kimataifa kwa michezo inayofanana na bao. Ni kundi la michezo kwa wachezaji wawili wanaohamisha kete (vijiwe, mbegu) kati ya nafasi zilizopangwa, mara nyingi mashimo katika bodi ya bao, ardhini au katika jiwe.



Michezo ya mankala inachezwa mahali pengi duniani. Inapendwa sana Afrika na Asia. Michezo hizi, zilitoka Africa.[1]
Kwa kawaida, watu wawili wanacheza. Wanaweka kete ndani ya shimo. Mchezaji mmoja anachagua shimo, anatoa kete, na anaziweka kwa shimo zingine moja kwa moja. Wachezaji wanajaribu kupata kete nyingi zaidi ili washinde. Lakina, kuna aina nyingi na kanuni tofauti za kukamata kete na kuziweka kwa shimo. Pia, michezo hizi za aina ya mankala zina idadi ya shimo tofauti. Lakini michezo hii yote ni michezo ya akili, na inasomesha watu kufanya hesabu. Kwa hivyo, watu wanapenda kuwafundisha watoto wao kucheza.
Remove ads
Jina la Mankala
Jina la Mankala linatumikakwa aina ya michezo tofauti, na kwa familia ya michezo. Jina hili ni la Kiarabu (منقلة), na linafanana na naqala (نقلة), yaani kuendelea.[2][3][4]
Soma pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads