Kivunjajungu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Vivunjajungu, vunjajungu au katamasikio ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Mantodea (mantis = nabii, eidos = umbo) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki na kusini (au kaskazini) kwa kanda za wastani. Kiwiliwili chao ni kirefu na chembamba. Miguu ya mbele imetoholewa kwa kukamata arithropodi wengine na hata vertebrata wadogo. Kwa kawaida koksa (coxa) za miguu ya wadudu ni fupi, lakini zile za miguu ya mbele ya vivunjajungu zimerefuka. Femuri na tibia zina miiba na meno inayowezesha mdudu kushika vizuri mawindo yake. Kama takriban wadudu wote vivunjajungu wana toraksi yenye sehemu tatu, lakini ile ya mbele, protoraksi, ni ndefu kuliko mbili nyingine pamoja na imeungwa vinamo na mesotoraksi. Hii inawezesha mdudu asogeze kichwa na miguu ya mbele pande zote wakati kiwiliwili kinatulia. Hata shingo ni kinamo na spishi kadhaa zinaweza kuzungusha kichwa kwa nyuzi 180.

Remove ads
Picha
- Amorphoscelididae (Myrmecomantis atra)
- Empusidae (Empusa pennata)
- Hymenopodidae (Hymenopus coronatus)
- Iridopterygidae (Bolbe sp.)
- Liturgusidae (Humbertiella similis)
- Mantidae (Miomantis caffra)
- Metallyticidae (Metallyticus splendidus)
- Sibyllidae (Sibylla pretiosa)
- Tarachodidae (Tarachodes sp.)
- Thespidae (Pogonogaster tristani)
![]() |
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kivunjajungu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads