Marehemu wote

From Wikipedia, the free encyclopedia

Marehemu wote
Remove ads

Marehemu wote ni adhimisho la baadhi ya madhehebu ya Ukristo kulingana na imani katika hali ya watu waliofariki dunia. Kwa baadhi yake ni suala la kuwakumbuka tu, kwa baadhi ni suala la kuwaombea pia [1].

Thumb
Siku ya marehemu wote, mchoro wa Jakub Schikaneder, 1888.

Ni muhimu hasa katika Kanisa la Kilatini (ambalo linaliadhimisha tarehe 2 Novemba[2], mara baada ya sherehe ya Watakatifu wote) na katika Ukristo wa mashariki (ambao linaliadhimisha mara kadhaa kwa mwaka, hasa kila Jumamosi, ambayo ndiyo siku ya Yesu kukaa kaburini kabla hajafufuka Siku ya Bwana).

Katika madhehebu hayo Kanisa, kama vile linashangilia kwa sifa za kufaa wanae wote wanaoshiriki tayari heri ya mbinguni, linawajibika pia kuziombea kwa Mungu roho za wale wote ambao walitangulia kuishi kadiri ya imani wakalala wakitumaini ufufuko na za wale wote ambao, tangu ulimwengu kuumbwa, Mungu tu alijua imani yao, ili kwa kutakaswa madoa yote ya dhambi, waingie ushirika wa mbinguni na kufurahia kumuona Mwenyezi Mungu alivyo [3].

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads