Margaret Clitherow

From Wikipedia, the free encyclopedia

Margaret Clitherow
Remove ads

Margaret Clitherow (1556 25 Machi 1586) alikuwa mwanamke Mwingereza ambaye, kwa ruhusa ya mume wake, alibadilisha imani yake ya dini kutoka Ushirika wa Anglikana kuingia Kanisa Katoliki.

Thumb
Margaret Clitherow, the Pearl of York.

Kwa vile aliwaficha mapadri nyumbani mwake na kuhudhuria misa ya Kikatoliki, alifungwa mara kadhaa katika dhuluma ya malkia Elizabeti I, akashtakiwa mahakamani lakini alikataa kujitetea ili asisababishe mahakimu wafanye dhambi ya kumpa adhabu ya kifo, hivyo akauawa kwa kubondwa mwili mzima na mzigo mkubwa [1].

Mwaka 1970 alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 25 Machi[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads