Matt Dallas
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Matthew Joseph "Matt" Dallas (amezaliwa tar. 21 Oktoba, 1982) ni mwigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kucheza uhusika wa katika mfululizo wa TV ya ABC Family Kyle XY.
Remove ads
Maisha ya awali
Dallas alizaliwa mjini Phoenix, Arizona, na alihitimu katika shule ya Arizona School for the Arts. Ana ndugu wawili wa kiume na mmoja wa kike.[1] Alianza kuwa na shauku ya uigizaji tangu akiwa na umri wa miaka 12, wakati bibi yake alivyomchukua katika utayarishaji wa tamthiliya ya The Ugly Duckling.
Kazi za sanaa
Dallas amecheza katika filamu kadhaa, vilevile uhusika katika mfululizo wa TV wa ABC Family, Kyle XY kwa misimu mitatu. Mfululizo uliisha mnamo tarehe 16 Machi, 2009 baada ya kukatwa na ABC. Dallas pia ameonekana katika Camp Slaughter (2005), Living The Dream (2006), na Babysitter Wanted (2008). Alikuwa mgeni kwenye kipindi cha TV cha Entourage.
Mwaka wa 2004, Dallas alionekana katika muziki wa video wa Fan, "Geek Love". Mwaka wa 2005, Dallas alicheza na Mischa Barton kwenye muziki wa video wa James Blunt wa "Goodbye My Lover" na mwaka wa 2008 alionekana katika muziki wa video wa Katy Perry, "Thinking of You".
Dallas alikuwa mshiriki kwenye TV mchezo wa ABC', Eastwick, alicheza kama kipenzi cha Roxie (Rebecca Romijn).[2] Mnamo 9 Novemba, 2009, ABC walikataa kuagiza vipengele vingine vya Eastwick, hatimaye mfululizo ukakatwa.[3] Mwaka wa 2009, ilitangazwa ya kwamba Dallas atacheza kwenye filamu ya Beauty and the Briefcase akiwa na Hilary Duff. Dallas alikuwa katika filamu za Kihindi-Kimagharibi iliyoitwa The First Ride of Wyatt Earp kama Bat Masterson, ambayo ilitolewa mnamo tarehe 6 Machi, 2012.
Remove ads
Maisha binafsi
Mnamo 6 Januari, 2013, Dallas alitangaza uchumba wake kupitia Twitter kuwa bwana wa Blue Hamilton, mwanamuziki.[4][5] Wameoana mnamo Julai 5, 2015.[6][7]
Filmografia
Filamu
Televisheni
Muziki wa video
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads