Mauzo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mauzo ni shughuli inayohusiana na kuuza au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa katika muda fulani.

Muuzaji humaliza kitendo cha uuzaji baada ya kujibu mwito wa ununuzi. Kuna kupitisha umiliki wa bidhaa na kulipa, ambapo kuna makubaliano ya bei ambayo italipiwa bidhaa ile. Muuzaji ndiye anayefanya tendo lile la uuzaji na uzo lile linaweza kumalizika kabla ya mnunuzi kumaliza kulipa.
Remove ads
Ufafanuzi
Mtu au shirika linaloonyesha nia ya kupata bidhaa ya thamani inayotolewa linajulikana kama mnunuzi au mteja mtarajiwa. Kununua na kuuza ni lile tendo la kubadilishana umiliki. Kununua ni kupokea umiliki wa kinachouzwa ilhali kuuza ni kupitisha umiliki kwa mnunuzi baada ya malipo. Muuzaji na mnunuzi huafikiana ili kukamilisha ubadilishaji wa thamani.[1]
Katika mauzo kunaweza kuwa na kujadiliana bei au bei inaweza kuwa isiyobadilika. Sanasana bei ya bidhaa au huduma hukuliwa na haja ya wanunuzi na wingi wake sokoni. Kwa biashara zinazolenga wanunuzi fulani, hasa matajiri, muuzaji anaweza kuiweka bei ya bidhaa bila kuzingatia bei ya ile bidhaa au huduma sokoni.
Remove ads
Mbinu
Mauzo yanaweza kuwa:[2]
- Ya moja kwa moja
- Yasiyo ya moja kwa moja
- Ya kupitia mawakala
- Ya rejareja
- Ombi la pendekezo
- Biashara kwa biashara[3]
- Ya kielektroniki
Mawakala wa mauzo
Mawakala katika mchakato wa mauzo wanaweza kuwakilisha upande wowote; kwa mfano:
- Wakala wa mauzo (kama vile kupitia mauzo shirikishi)
- Wakala mnunuzi
- Wakala anayewakilisha pande zote mbili
- Wakala wa kuangalia shughuli tu
- Uwakilishi wa nje wa mambo ya mauzo
- Msimamizi wa mauzo wa kutekeleza mikakati ya mauzo na kuratibu idara ya mauzo
- Mfanyabiashara muuzaji
- Wataalamu wa mauzo mtandaoni
Aina za uuzaji
- uso kwa uso (P2P)
- uso kwa biashara (P2B)
- biashara kwa biashara (B2B)
Aina za mauzo kijiografia
- mauzo ya ndani
- mauzo ya serikali
- mauzo ya nchi
- mauzo ya kimataifa[4]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads