Maximilian Kolbe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Maximilian Maria Kolbe (8 Januari 1894 – 14 Agosti 1941) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Polandi.

Katika historia ya Kanisa anajulikana kwa jinsi allivyomheshimu Bikira Maria kwa jina la Imakulata, yaani Mkingiwa dhambi ya asili.
Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma (Italia) na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Unazi sehemu mbalimbali na hatimaye katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Huko alijitoa kafara ya upendo na uaminifu kwa Mungu na binadamu kwa kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu[1].
Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Oktoba 1971, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu mfiadini tarehe 10 Oktoba 1982.
Remove ads
Sala yake
Wewe umenipenda milele, tangu u Mungu; hivyo umenipenda na utanipenda milele!...
Upendo wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo, na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads