Melissa McCarthy
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Melissa Ann McCarthy (amezaliwa Agosti 26, 1970)[1] ni mwigizaji filamu, mchekeshaji, mwandishir, na vilevile mtayarishaji kutoka nchini Marekani.
McCarthy alianza kupata umaarufu kwa uhusika wake wa Sookie St. James kwenye mfululizo wa TV wa Gilmore Girls (2000–2007). Kwenye ucheshi wa ABC Samantha Who? (2007–2009), amecheza kama Dena. Halafu baadaye akaja kucheza kama Molly Flynn kwenye ucheshi wa CBS Mike & Molly, uhusika ambao umempatia tuzo ya Primetime Emmy Award for Outstanding Lead Actress in a Comedy Series,[2] vilevile kupata kuchaguliwa mara mbili katika mifululizo iliyofuata hapo baadaye.
Vilevile amechaguliwa (bila kushinda) kwa ajili ya tuzo za Primetime Emmy Award for Outstanding Guest Actress in a Comedy Series kwa kazi yake kama mtangazaji wa Saturday Night Live kwa miaka mitatu mfululizo.
McCarthy alianza kupata mafanikio yake makubwa zaidi baada ya kucheza uhusika wake wa Megan Price kwenye filamu ya vichekesho ya mwaka wa 2011 Bridesmaids, ambayo imepelekea kupata kuingizwa katika tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na Academy Award kwa ajili ya Best Supporting Actress, BAFTA na Screen Actors Guild Award zote kwa ajili ya Best Supporting Actress.[3] Mwaka wa 2013, ameshitiki katika filamu ya vichekesho maarufu kama Identity Thief na The Heat. Pia ameonekana katika filamu kama vile The Nines, The Back-up Plan, Life as We Know It and The Hangover Part III. Mwaka wa 2014, McCarthy amecheza katika filamu ya vichekesho Tammy na igizo la St. Vincent.[4] Mwaka wa 2015, amekuwa gumzo katika magazeti mengi duniani kwa kucheza filamu ya mapigano ya Spy. Yeye ndiye mwanzilishi wa kampuni ya filamu ya On the Day Productions akiwa na mumewe Ben Falcone.
Remove ads
Maisha ya awali
McCarthy alizaliwa mjini Plainfield, Illinois,[5] akiwa kama binti wa Sandra na Michael McCarthy.[6][7] Huyu ni binamu wa mwigizaji na mwanamitindo Jenny McCarthy.[8] McCarthy alilelewa katika "shamba kubwa familia ya Katoliki ya Eire".[9][10] Moja kati ya mababu zake wana asili ya County Cork.[11] Alihitimu katika chuo cha St. Francis Academy (sasa kinaitwa Joliet Catholic Academy) huko mjini Joliet, Illinois.[12] Kazi yake ilianza na uchekeshaji wa wima.[13] McCarthy ni mhitimu wa The Groundlings, mahali pa kufundishi ucheshi huko mjini Los Angeles, California.[14]
Remove ads
Kazi
1997–2010

Maisha binafsi
McCarthy ameolewa na mshikaji wake wa zamani, Ben Falcone, mwigizaji na mhitimu wa The Groundlings, mnamo Oktoba 8, 2005.[15][16] Falcone anafanya mionekano kadha wa kadha katika filamu anazocheza McCarthy, kama vile Bridesmaids, The Heat, Tammy, Identity Thief na Spy. Kwa pamoja, wana mabinti wawili; wa kwanza kazaliwa 2007 na mwingine 2010.[17][18]
Filmografia
Filamu
Televisheni
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads