Metodi wa Olimpo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Metodi wa Olimpo (alifariki mwaka 311 hivi) alikuwa askofu wa Olimpo (Lycia) na mfiadini kutoka Anatolia (leo nchini Uturuki)[1].

Taarifa za kwanza juu yake ziliandikwa na mtakatifu Jeromu[2]
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Maandishi
Metodi aliandika sana na kwa ufasaha kuhusu masuala ya teolojia, akipinga uzushi wa wakati wake na hasa ule wa mafundisho kadhaa ya Origen.
Kwa bahati mbaya, vitabu vyake vimepotea kwa kiasi kikubwa. Kilichotufikia kizima kwa Kigiriki kinahusu ubikira (Symposion e peri hagneias).[4]
Kati ya matoleo ya maandishi yake kuna: Patrologia Graeca, XVIII; Jahn, S. Methodii opera et S. Methodius platonizans (Halle, 1865); Bonwetsch, Methodius von Olympus: I, Schriften (Leipzig, 1891).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
