Metras
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Metras (aliuawa 249) alikuwa mfiadini Mkristo wa Aleksandria (Misri) ambaye kwa kukataa kutamka maneno yasiyofaa aliuawa kwa kupigwa mawe wakati wa dhuluma ya kaisari Decius [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Januari[2][3].
Pengine wanatajwa kama wafiadini wenzake Saturnini, Tirso, Vikta, Tarsisi, Zotiko na Siriaki[4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads