Mhandisi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mhandisi (kutoka neno la Kiarabu) ni mtu mwenye elimu sahihi katika taaluma ya uhandisi. Jina la Kiingereza engineer (kwa Kiswahili: injinia) linatoka kwenye Kilatini ingenium, maana yake ni "uerevu".

Wahandisi hubuni miundo, mashine na mifumo huku wakizingatia mapungufu yaliyowekwa na ufanisi, usalama na gharama. Kazi nyingi zinatumika sayansi, kwa kutumia habari iliyotolewa na wanasayansi kufanya kazi zao. Mbali na kufanya kazi na vitu, mhandisi lazima pia kuwa mzuri katika kufanya kazi na watu na pamoja na fedha.
Remove ads
Ufafanuzi
Sheria ya Wahandisi ya Kenya inafafanua kuwa mhandisi ni mtu anayetoa huduma zinazohusiana na upembuzi yakinifu, upangaji, uchunguzi, usanifu, mchoro wa awali, michoro, vipimo, ujenzi, uzinduzi rasmi, utendaji kazi, matengenezo, usambazaji wa vifaa maalum vya uhandisi na usimamizi wa kazi au miradi ya uhandisi. Mhandisi pia anaweza kufanya kazi zinazojumuisha utoaji wa huduma za kitaalamu, ushauri, uchunguzi, tathmini, upangaji, usanifu au uwajibikaji wa usimamizi wa ujenzi, uendeshaji au matengenezo yanayohusiana na huduma za umma zinazomilikiwa na serikali au sekta binafsi, majengo, mitambo, vifaa, michakato, kazi au miradi ambayo utekelezaji wake unahitaji matumizi ya kanuni za uhandisi na takwimu husika [1].
Mhandisi hutumia ujuzi wake wa sayansi na hisabati kuchanganua shida na hatimaye kubuni suluhu. Anahitajika kuwa na uwezo wa kutumia sayansi ya kiuhandisi kusimaia kazi za kiufundi. Kazi yake kimsingi ni ya kiakili na yenye upeo mpana, na si ya kimaumbile ya kurudia-rudia kiakili au kimwili[2].
Remove ads
Kazi za mhandisi
Uchanganuzi na utafiti
Wahandisi hutumia ujuzi wa kisayansi kutafiti mbinu mbalimbali za kusuluhisha matatizo. Pia wanahusika katika kuchanganua suluhu katika majaribio, utekelezaji au matengenezo.
Ubunifu na upangaji
Wajibu mkuu wa mhandisi ni kutumia sayansi kubuni suluhu na kupanga jinsi itakavyotekelezwa. Upangaji hufanywa kwa usanifu, michoro, kupima na uundaji wa modeli kwa kutumia kanuni za hisabati au programu za tarakilishi.
Usimamizi
Mhandisi hutwikwa jukumu la
- kupanga, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya uhandisi katika sekta ya umma au binafsi;
- kuhakikisha kwamba michakato, kazi na shughuli zote za uhandisi zinafuata viwango vilivyowekwa na kanuni za kitaalamu;
- kutoa uongozi wa kiufundi kwa wahandisi wengine, mafundi na watendaji katika mradi husika;
- kusimamia matumizi bora ya rasilimali, gharama na muda katika utekelezaji wa miradi ya uhandisi;
- kuhakikisha usalama wa wafanyakazi, umma na mazingira katika hatua zote za uhandisi.
Remove ads
Taaluma
Kitaalamu, wahandisi huainishwa katika ngazi tatu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki[3][1].
Mhandisi Mhitimu
Huwa ni mhandisi aliyehitimu, ila hana tajriba ya uhandisi. Kwa kawaida, anahitajika apitie kipindi cha miaka miwili au mitatu, kulingana na sheria ya nchi, cha uanagenzi. Katika kipindi hicho, yeye huhusishwa katika kazi ya uhandisi chini ya usimamizi wa mhandisi mtaalamu.
Mhandisi Mtaalamu
Mhandisi hutawazwa kuwa mtaalamu au msajiliwa baada ya kupitia kipindi cha uanagenzi na kufaulu katika mtihani wa tathmini ya kitaalamu unaoendeshwa na Bodi. Katika ngazi hii, mhandisi hupewa mamlaka kamili ya kujisimamia kitaaluma na muhuri wa kuidhinisha kazi za kiuhandisi.
Mhandisi Mshauri
Mshauri ni mhandisi aliyekomaa katika taaluma yake. Kazi yake inajumuisha huduma za ushauri na mashauriano zinazohusiana na kazi, huduma au bidhaa za kitaalamu za uhandisi .
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads