Muhogo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Muhogo (Kiing. cassava) ni mmea wa jenasi Manihot na chakula muhimu katika Afrika, Amerika Kusini na nchi za Asia Kusini. Sehemu ya kuliwa ni hasa viazi vyake (mizizi minene au mahogo) vilivyo na wanga nyingi halafu pia majani yake yenye protini na vitamini.
Remove ads
Sumu ndani ya aina za muhogo
Kuna aina kadhaa za muhogo zinazotofautiana hasa katika kiwango cha sianidi (cyanide) ndani yake. Sianidi ni sumu inayoandaliwa ndani ya mmea kwa umbo la kemikali linamarin. Linamarin hubadilika kuwa sianidi.
Viwango vya sianidi vinatofautiana kati ya spishi mbalimbali za muhogo. Aina zenye kiwango kidogo sana hazina matatizo lakini kwa jumla zao linatakiwa kuandaliwa kabla ya kuliwa.
Dawa ya sianidi hupotea kwa kuacha mizizi katika maji kwa siku mbili tatu. Njia nyingine ni upishi kwa joto kali kwa mfano kukaanga katika mafuta. Njia nyingine inayotumiwa hasa Afrika ya Magharibi ni kusaga viazi na kukoroga unga katika maji; baada ya masaa kadhaa maji hubadilishwa na uji unapikwa kuwa aina ya ugali.
- Maua
- Matunda
- Mahogo
- Vipande vya muhogo
- Ndugu ya muhogo (Manihot palmata)
- Manihot esculenta - Museum specimen
![]() |
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muhogo kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads