Mikosi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mikosi
Remove ads

Mikosi, ni jina la albamu ya kwanza kutoka kwa kundi zima la muziki wa hip hop la Temeke Dar es Salaam, Tanzania maarufu kama G.W.M. Albamu imetoka mwaka wa 2000 - ukiwa mwaka wa matoleo mengi ya albamu za hip hop ya Tanzania kutoka. Hamasa ya kutoa albamu na kufanya uzinduzi zama hizi ndiyo hasa zilitamba. G.W.M ni moja kati ya makundi yanayoheshimika katika miaka ya 1990.

Ukweli wa haraka Studio album ya G.W.M, Imetolewa ...

Walikuwa kufahamika haraka nchini Tanzania kwa ujuvi wao wa utunzi wa mashairi ulioendana na wakati ule. Walianza kutamba mwaka 1995 baada ya kutoa wimbo wa "Cheza mbali na kasheshe". Albamu hii ilitakiwa itoke tangu miaka ya 1990, lakini mipango ya kusaini mkataba wake ilienda kombo na kuja kutoka mwaka wa 2000, mbele kidogo baada ya kuvuma kwa sana. KR baaaye akajiunga na kundi la muda mfupi la Wachuja Nafaka. Nyimbo za katika albamu zilitayarishwa na Bonny Luv na Rajabu Marijani.

Remove ads

Orodha ya nyimbo

Thumb
Zama zile ilikuwa lazima utie saini katika kila kanda itakayotoka ili kuonesha uhalali wa usambazwaji huo. Hii ni moja kati ya mihuri ya GWM iliyoonesha kuidhinishwa kwa kazi hii. Ingawa kulikuwa na malalamiko mengi sana juu ya uhujumu wa mauzo ya kanda kwa wakati huo.

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatika katika albamu hii na maelezo yake ya msingi.

Maelezo zaidi Upande, Jina la wimbo ...
Remove ads

Kikosi kazi

Viungo vya Nje

  • Mikosi katika wavuti ya Discogs
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads