Mizari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mizari (lat. & ing. Mizar pia ζ Dzeta Ursae Majoris, kifupi Dzeta UMa, ζ UMa) ni kati ya nyota angavu katika kundinyota ya Dubu Mkubwa (Ursa Major). Ina umaarufu kama nyota maradufu inayoonekana kwa macho matupu.
Remove ads
Jina
Mizari ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka Waarabu wanaosema المئزر al-mizar inayomaanisha "kimori, aproni" [3]
Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Mizar" [4].
Dzeta Ursae Majoris ni jina la Bayer; Dzeta ni herufi ya saba katika alfabeti ya Kigiriki lakini Mizari ni nyota angavu ya nne na hii ni mfano ya kwamba Bayer hakufuata mwangaza kamili wakati wa kuorodhesha nyota.
Remove ads
Tabia
Mizari ipo kwa umbali wa miaka nuru takriban 86 kutoka Jua letu. Mwangaza unaoonekana ni mag 2.27. Mtu mwenye macho mema anatambua kando yake nyota dhaifu zaidi inayoitwa Alcor hivyo Mizar na Alcor ni jozi maarufu ya nyota. Haijulikani bado kama ni nyota Maradufu hali halisi zilizoungwa pamoja kwa gravity au la.
Lakini kwa darubini Mizar yenyewe ilitambuliwa kuwa nyota maradufu. Galileo Galilei aliweza kuona sehemu zake mbili alipokuwa mtu wa kwanza wa kutazama nyota kwa darubini. Sehemu hizi mbili zinaitwa Mizari A na Mizari B.
Kwa kutumia darubini bora zaidi ilitambuliwa katika karne ya 19 ya kwamba Mizar A ni nyota mbili pia. Leo hii inajulikana kuwa Mizar ni mfumo wa nyota nne zinazoshikamana na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Kwa jumla ni ni jozi mbili za nyota yaani Mizar A 1+2 na Mizar B 1+2.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya Nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads