Mkoa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa ni eneo fulani ndani ya nchi ambalo ni ngazi ya utawala wa nchi ile. Matumizi ya jina hilo yanaweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Kwa kutafsiri vitengo vya utawala vya nchi mbalimbali wakati mwingine kuna mchanganyiko wa maneno "mkoa", "wilaya" na "jimbo" hasa kwa sababu matumizi ya maneno yanayolingana na ya Kiingereza "region", "district" na "province" hayafuati kila mara utaratibu maalumu.
Remove ads
Mikoa ya Tanzania
Katika Tanzania mkoa ni ngazi ya utawala chini ya serikali ya kitaifa hivyo ni kitengo cha ngazi ya kwanza; ndani ya mkoa kuna wilaya kama mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa.
Mikoa hii huwa ni vitengo vya utawala wa serikali kuu, si maeneo yenye madaraka ya kujitawala na viongozi wanaochaguliwa kwa kura. Kiongozi wa mkoa ni Mkuu wa Mkoa anayeteuliwa na rais wa taifa.
Utaratibu huo nchini Kenya umefutwa na katiba mpya ya mwaka 2010.
Remove ads
Mikoa chini ya majimbo
Nchi zenye muundo za shirikisho zinakuwa na majimbo au madola ndani ya taifa na kila jimbo au dola la shirikisho linaweza kuwa na mikoa yake ambayo ni ngazi ya pili katika mfumo huu. Ila tu si lazima kuwa na mikoa: kuna pia wilaya moja kwa moja chini ya majimbo au madola ya shirikisho kama ngazi ya pili bila kutumia ngazi ya mikoa tena.
Mfano wake ni Ujerumani ambako majimbo mengi huwa na ngazi za mkoa na chini yake wilaya na miji.
Kuna pia nchi zenye majimbo ya kiutawala yanayogawiwa kwa mikoa. Mfano wake ni China ambako majimbo hutawaliwa na viongozi kwa niaba ya serikali kuu na majimbo yale huwa na mikoa na wilaya kama ngazi za chini.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkoa kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads