Mkuku (kundinyota)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkuku (kundinyota)
Remove ads

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Mkuku

Thumb
Nyota za kundinyota Mkuku (Carina) katika sehemu yao ya angani

Mkuku (kwa Kilatini na Kiingereza Carina) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Jina

Carina (Mkuku) ilianzishwa kama kundinyota la pekee katika karne ya 18 kwa hiyo haikujulikana vile kwa mabaharia Waswahili ambayo hata hivyo waliotumia nyota zake kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2]

Hadi karne 19 kundinyota hili lilitazamiwa kuwa sehemu ya kundinyota kubwa zaidi lililoitwa Argo Navis, mara nyingi pekee "Navis" (yaani merikebu) iliyokuwa moja ya makundinyota 48 yaliyoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio. Waarabu waliita Safina au Markab. Lacaille alihesabu ndani yake nyota 180 zilizokuwa nyingi mno kwa kuzitaja kwa majina ya Bayer na hivyo alianza tayari kugawa Argo Navis kwa sehemu tatu za Tanga (Vela), Shetri (Puppis) na Mkuku (Carina). Hii ilithibitishwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya makundinyota 88 ya kisasa yaliyotolewa mwaka 1930. [3] [4]

“Carina” inataja mkuku ambao ni sehemu ya chini kabisa ya chombo cha majini.

Remove ads

Mahali pake

Mkuku - Carina iko katika ukanda wa Njia Nyeupe, karibu na kundinyota la Salibu (Crux), si mbali na ncha ya anga ya kusini.

Inapakana na kundinyota jirani ya Kinyonga (Chamaeleon), Nzi (Musca), Kantarusi (Centaurus), Tanga (Vela), Shetri (Puppis), Mchoraji (Pictor) na Panzimaji (Volans).

Nyota

Mkuku - Carina ni kundinyota kubwa lenye nyota nyingi. Suheli (Carina) au α Carinae ni nyota angavu sana , ni ya pili kwenye anga ya usiku baada ya Shira (Sirius). Ina mwangaza unaoonekana wa mag -0.72 ikiwa umbali wa miakanuru 310 na Dunia[5][6].

Eta Carinae ni nyota maradufu ya nyota mbili au zaidi iliyowaka ghafla mwaka 1843 ikaonekana angavu kushinda Suheli[7]. Sasa nyota zake zimo ndani ya nebula Homunculus ambayo ni wingu angavu lililobaki baada ya mlipuko wa supanova ile. [8]


Maelezo zaidi Jina la (Bayer), Namba ya Flamsteed ...


Tanbihi

Viungo vya Nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads