Moluska

From Wikipedia, the free encyclopedia

Moluska
Remove ads

Moluska ni wanyama wasio na mifupa ambao wanaishi zaidi majini, ambamo ni asilimia 23 za wanyama wote walioainishwa. Lakini wengine wanaishi katika nchi kavu, kama vile konokono wengi. Baharini wako pia kama kome na chaza.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Siku hizi kuna spishi 85,000 za wanyama hao, nazo ni tofauti sana. Spishi nyingine zimekoma.

Jina lilienea kuanzia Kifaransa mollusque, kutoka neno la Kilatini molluscus, ambalo mzizi wake ni mollis, yaani laini. Aristotle aliwahi kutumia neno la Kigiriki τα μαλακά, ta malaka, "vitu laini", kwa aina ya mnyama wa baharini wa jamii ya pweza.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads