Mrisho Ngassa
Mwanasoka wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mrisho Ngassa (alizaliwa tarehe 5 Mei 1989) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Tanzania ambaye aliichezea klabu ya Ndanda FC na pia yanga African pia aliichezea timu ya taifa ya Tanzania.
Remove ads
Majaribio West Ham United
Mwezi wa Aprili 2009, Ngassa kutokana na uchezaji wake mzuri alialikwa na klabu ya Uingereza iitwayo West Ham United kwa majaribio ya wiki mbili ili waweze kumnunua, majaribio yalipoisha West Ham ilizungumzwa kuwa ni mchezaji mzuri ila anahitaji baadhi ya vitu fulani navyo ni vya kiufundi katika mambo ya mpira hata hivyo inazungumzwa kuna baadhi ya klabu barani Ulaya zinapendelea kumchukua.
Timu ya Taifa ya Tanzania
Katika mashindano ya Cecafa 2009 yaliyofanyika Kenya alijinyakulia ubingwa wa mfungaji bora katika mashindano hayo kwa kuweza kufunga mabao ma 5 katika shindano hilo lakini timu yake ya taifa ya Tanzania ilichukua nafasi ya Nne katika mashindano hayo.
Ngassa ni kijana ambae anaangaliwa kua atakua na mustakabali mzuri wa nchi yake na Afrika pia. 21 Mei 2010 alijiunga na Azam FC baada ya majaribio.
Mnamo Julai 2011 alijaribiwa na Seattle Sounders akaja kama mchezaji dhidi ya Manchester United katika mechi ya kirafiki. Baada ya muda alijiunga na kikosi cha Simba S.C.
Remove ads
Viungo vya nje
- Kuhusu Mrisho Ngassa katika tovuti ya Goalzz.com
- Majaribo na West Ham Ilihifadhiwa 4 Mei 2009 kwenye Wayback Machine. Kiingereza
- kuhusu majaribo hayo katika Tovuti mashuhuri ya BBC Sport. 1 Aprili 2009 Retrieved 29 Mei 2009
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads