Msomaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Msomaji ni mtu anayesoma maandishi fulani, hasa vitabu. Kwa njia hiyo anapokea ujumbe kutoka kwa waandishi.

Katika Ukristo


Katika Ukristo ni hasa jina la mtu anayesoma kutoka katika Biblia wakati wa ibada, akiwa amejiandaa kutoa huduma hiyo kwa kiwango cha ubora ili Neno la Mungu lisikike vizuri.
Katika Kanisa la Kilatini
Katika Kanisa la Kilatini na baadhi ya madhehebu mengine, waumini wanaweza kukabidiwa huduma hiyo kwa namna ya kudumu.
Hasa wanaojiandaa kupata ushemasi na upadri wanatakiwa kupitia kwanza usomaji na usindikizi kama matayarisho kwa daraja takatifu hizo.
Kuanzia mwaka 2021 wanawake pia wanaweza kupewa kazi hiyo, baada ya Papa Fransisko kurekebisha kanuni 230 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa.
Viungo vya nje
- Church Reading: A Vital Ministry Ilihifadhiwa 25 Januari 2010 kwenye Wayback Machine. by Deacon Sergius Halvorsen (Orthodox)
- Photo: Tonsure of a Reader
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads