Akoliti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Akoliti (kwa Kiingereza "acolyte", kutoka Kigiriki ἀκόλουθος, akoluthos, yaani "msindikizaji") ni Mkristo anayemsaidia askofu, padri au shemasi anapoongoza ibada fulani[1].



Katika Kanisa la Kilatini
Katika Kanisa la Kilatini tangu mwaka 1972, pamoja na usomaji, ni mojawapo kati ya huduma mbili za lazima[2] ambazo wale wote wanaojiandaa kupata daraja takatifu wazipate na kuzitekeleza kwa muda fulani.
Kati ya kazi muhimu za akoliti, mojawapo ni kuwagawia waamini wenzake sakramenti ya ekaristi[3].
Kuanzia mwaka 2021 wanawake pia wanaweza kupewa kazi hiyo, baada ya Papa Fransisko kurekebisha kanuni 230 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads