Fabaceae

Mmea jamii ya mkunde From Wikipedia, the free encyclopedia

Fabaceae
Remove ads

Fabaceae au Leguminosae, inayojulikana kama familia ya mimea ya jamii ya mkunde na mimea aina ya mharagwe, ni familia kubwa ya mimea yenye maua iliyo na umuhimu kiuchumi na kibiolojia. Familia hii inajumuisha miti, vichaka na mimea ya muda na ya msimu, na inatambuliwa kwa urahisi kwa kupitia matunda (kunde) na majani yake. Mimea mingi ya jamii ya mkunde ina maua na matunda ya kipekee.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Familia hii imesambaa maeneo mengi duniani na ni familia ya tatu kwa ukubwa kwa mimea ya nchi kavu kwa kuzingatia idadi ya spishi, ikipitwa na familia ya Okidi na Asteraceae pekee. Inajumuisha takribani jenasi 751 zenye spishi zipatazo 19,000. [1] [2]

Jenasi tano kubwa zaidi za familia hii ni Astragalus (zaidi ya spishi 3,000), Acacia (spishi zaidi ya 900), Indigofera (karibu spishi 700), Crotalaria (spishi karibu 700), na Mimosa (karibu spishi 400). Jenasi hizi kwa pamoja zinabeba walau robo ya spishi zote za mimea ya jamii ya mkunde. Spishi 19,000 za jamii ya mkunde zinazojulikana hadi sasa kwa pamoja zinatengeneza karibu 7% ya spishi zote za mimea yenye maua. [3] Mimea ya familia hii ndiyo inayopatikana kwa wingi zaidi katika misitu ya mvua ya kitropiki na misitu kavu ya Amerika na Afrika. [4]

Tafiti za hivi karibuni zilizotumia njia za kimolekula na maumbile zinaonyesha kwamba familia ya Fabaceae ni kundi la kijenetiki kutoka kwa mhenga mmoja. [5] Swala hili linapata mkazo kutokana na uhusiano kati ya makundi ya mimea ndani ya familia hii, uhusiano wa familia hii mimea inayokaribiana nayo pamoja na tafiti za jenetika zinazotumia Asidi Kiinideoksiribo.[6][7][8]. Tafiti hizi zimeonyesha kwamba mimea ya familia ya Fabaceae ni kundi lenye jadi moja linalohusiana kwa ukaribu na familia za Polygalaceae, Surianaceae na Quillajaceae ambazo kwa pamoja zipo chini ya oda ya Fabales.[9]

Baadhi ya mimea ya familia ya Leguminosae imekua chanzo kikuu cha chakula cha binadamu kwa milenia nyingi pamoja na nafaka, baadhi ya matunda na vyakula vya mizizi vya kitropiki. Matumizi ya vyakula hivi yanahusiana kwa ukaribu na mageuko ya binadamu.[10] Familia hii inajumuisha mimea mingi yenye umuhimu kwanye kilimo na chakula, ikiwemo Glycine max (maharagwe ya soya), Phaseolus (maharagwe), Pisum sativum (njegere), Cicer arietinum (njegere kubwa), Medicago sativa (luseni), Arachis hypogaea (karanga), Ceratonia siliqua (karuba), na Glycyrrhiza glabra. Spishi nyingine za familia hii zinatambulika kama magugu sehemu mbali mbali duniani zikiwemo: Cytisus scoparius, Robinia pseudoacacia, Ulex europaeus, Pueraria montana, na baadhi ya spishi za jenasi Lupinus.

Remove ads

Maana na chanzo cha jina

Jina 'Fabaceae' linatokana na jenasi ya zamani Faba ambayo kwa sasa ipo ndani ya jenasi Vicia. Neno "faba" linatoka kwenye kilatini, maana yake nyepesi ikiwa ni "haragwe". Leguminosae ni jina la zamani ambalo bado linakubalika ambalo linaelezea tunda la mimea ya familia hii, ambayo inaitwa legumes kwa jina la kiingereza.

Uainishaji wa kisayansi

Fabaceae imewekwa katika oda ya Fabales kulingana na mifumo mingi ya uainishaji, ukiwemo mfumo wa APG III. Kwa sasa, familia hii inajumuisha nusufamilia sita: [11]

  • Caesalpinioideae : jenasi 148 na takribani spishi 4400. Imeenea zaidi kwenye hali za kitropiki, mfano Caesalpinia, Senna, Mimosa, Acacia . Inajumuisha familia ya zamani ya Mimosoideae (jenasi 80 na spishi takribani 3200; hupatikaana haswa kwenye hali za kitropiki, na ukanda wa Asia na Amerika wenye joto kiasi (temperate)
  • Cercidoideae: jenasi 12 na spishi takribani 335. Hupatikana zaidi kwenye hali za kitropiki. Bauhinia, Cercis .
  • Detarioideae : jenasi 84 na spishi takribani 760. Imeenea zaidi kwenye hali za kitropiki. Amherstia, Detarium, Tamarindus .
  • Dialioideae : jenasi 17 na spishi takribani 85. Imeenea katika maeneo ya tropiki. Dialium .
  • Duparquetioideae : jenasi 1 na spishi 1. Inapatikana Afrika Magharibi na Kati. Duparquetia .
  • Faboideae (Papilionoideae) [12]): genera 503 na spishi ~ 14,000. Hupatikana maeneo mengi. Mfano: Astragalus, Lupinus, Pisum.
Remove ads

Maelezo

Mimea ya familia ya Fabaceae ipo kwenye makundi mbali mbali kuanzia miti mikubwa (kama Koompassia excelsa) au mimea ya majani ya msimu. Hata hivyo mimeo mingi kwenye familia hii ipo kwenye kundi la mimea ya kudumu isiyo ya miti. Maua ya mimea ya familia hii hua madogo kwenye mfumo wa inflorescences japo wakati wingine ua hubaki moja. Uchavushaji wa maua yake huzaa matunda aina ya mikunde.

Ukuaji

Familia ya Fabaceae ina aina nyingi tofauti za ukuaji, zikiwemo, kama miti, vichaka au mimea ya kutambaa na kupanda. Mimea ya familia hii isiyo ya miti inaweza kua ya msimu au muda mrefu, bila mkusanyiko wa majani ya chini au mwisho. Mimea mingi ya jamii ya mikunde ina kamba kamba (tendrils) ambazo husaidia mmea kushishikiza. Inaweza kusimama wima yenyewe, kukua juu ya mimea mingine (epiphytic) au kutanda/kutambaa. Ile inayotambaa hua inajishikilia kwa matawi yake au kamba kamba (tendrils). Mimea ya jamii hii inaweza kua ambayo inaweza kuvumilia ukame, inayopenda maji au ile inayoweza kuishi mazingira mengi. [13][14]

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads