Mto Bell
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mto Bell ni mto wa Afrika Kusini ambao unapokea maji yake kutoka nyanda za juu za Drakensberg mashariki katika jimbo la Rasi Mashariki. Beseni yake ya utiririshaji inakadiriwa kuwa ni eneo la kilomita za mraba 424 ikianza kwenye kimo cha mita 3,001 juu ya usawa wa bahari na kushuka hadi mita 1720.
Chanzo cha mto kiko karibu na mpaka wa Lesotho (30°40′34″S 28°08′33″E). Kwa kushuka unapitia mji wa Rhodes, hadi kuungana na Mto Sterkspruit na kuanzia hapa yote miwili huitwa Mto Kraai (30°51′08″S 27°46′43″E) unaoishia katika Mto Orange (30°40′4″S 26°45′9″E).
Mto una idadi kubwa ya samaki aina ya trout. Kila mwaka kuna mashindano ya siku tatu ambako hadi washiriki 80 hushiriki kuvua samaki kwa siku tatu kwenye mwendo wa mto kwa kilomita 180.
Eneo maji yanapokusanyika mlimani lilitumiwa kwa ajili ya shughuli za malisho ya mifugo tangu miaka ya 1870.[1] Hii imesababisha mmomonyoko wa ardhi kwenye ufuko na kuathiri ubora wa maji ya mto Bell.Ili kutatua tatizo hilo jamii ya mimea ya Salix, hasahasa Salix caprea, zimekuwa zikipandwa pembezoni mwa kingo za mto ili kuzuia mto usije kuhama.[2]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads