Lesotho

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lesotho
Remove ads

Ufalme wa Lesotho, au Lesotho, ni nchi ndogo inayozungukwa na Afrika Kusini pande zote. Haina pwani kwenye bahari yoyote.

Ukweli wa haraka


Thumb
Malealea, mandhari ya Lesotho

Jina Lesotho lamaanisha eneo la Basotho (wakazi 99.7%), watu ambao wanaongea lugha ya Kisotho, ambayo ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Wakati wa ukoloni ilijulikana kama Basutoland.

Sasa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Ina wakazi milioni 2 hivi.

Mji mkuu ni Maseru.

Remove ads

Jiografia

Makala kuu: Jiografia ya Lesotho
Thumb
Theluji kwenye barabara ya Lesotho

Ukweli wa kijiografia ambao wajulikana zaidi kuhusu Lesotho ni kwamba ni nchi inayozungukwa na Afrika ya Kusini, na ni nchi huru pekee duniani ambayo yote iko juu ya mita 1,000 juu ya usawa wa bahari (UB) (ft 3,281). Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (futi 4,593), na zaidi ya asilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (futi 5,906).

Remove ads

Historia

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Lesotho ya sasa ilianza kupatikana mwaka 1822 chini ya chifu Moshoeshoe I aliyeungana na makabila mengine dhidi ya Shaka Zulu (1818-1828).

Baadaye nchi iliathiriwa na mahusiano na Waingereza na Makaburu wa . Koloni la Rasi (leo Afrika Kusini), yakiwemo mapigano ya mara kwa mara.

Wamisionari walioalikwa na Mfalme Moshoeshoe I walianza kuandika na kuchapa kwa lugha ya Kisotho kati ya miaka 1837 na 1855.

Mwaka 1867 nchi ikawa chini ya malkia wa Uingereza kwa jina la Basutoland lakini mwaka 1869, Waingereza waliwaachia Makaburu nusu ya eneo la Basutoland.

Uhuru ulipatikana tena mwaka 1966, na nchi ikaitwa ufalme wa Lesotho.

Remove ads

Wilaya

Thumb
Wilaya.
Makala kuu: Wilaya za Lesotho

Kwa usimamizi wa serikali, Lesotho imegawiwa katika wilaya 10, kila moja ikiongozwa na Karani wa wilaya.

Kila wilaya ina mji unaoitwa mji wa kambi (camptown).

  • 1 Berea
  • 2 Butha-Buthe
  • 3 Leribe
  • 4 Mafeteng
  • 5 Maseru
  • 6 Mohale's Hoek
  • 7 Mokhotlong
  • 8 Qacha's Nek
  • 9 Quthing
  • 10 Thaba-Tseka

Watu

Thumb
Nyumba nchini Lesotho

Wakazi kwa asilimia 90 ni Wakristo, wakigawanyika karibu sawa kati ya Wakatoliki na Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali.

Utamaduni

Thumb
Mto Makhaleng, mabonde kwa milima ya Lesotho
Thumb
Malealea, magharibi mwa Lesotho
Thumb
Bonde nchini Lesotho

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Uchambuzi


Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lesotho kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads