Mto Blood
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mto Blood (pia: Bloedrivier, Ncome, yaani "mto wa damu") upo katika eneo la KwaZulu-Natal, Afrika ya Kusini.

Huu mto una vyanzo vyake Kusini-mashariki mwa Utrecht; ukiacha vilima imeunganishwa na matawi mawili vinapoanzia Schurveberg, ambapo baada ya hapo hutiririka ikienea katika tambarare za mchanga.[1]
Mto Blood ni tawimto la Mto Buffalo, ambayo ni tawi la Mto Tugela unaojiunga kutokea kaskazini-mashariki.[2]
Mto huu umepata jina lake kutokana na mapigano baina jeshi la mfalme Mzulu Dingaan na kundi la makaburu chini ya Andries Pretorius yaliyotokea tarehe 16 Desemba 1838 ambako maji ya mto yamekuwa mekundu kutokana na damu ya Wazulu.
Upande wa kusini-magharibi wa mji wa Vrijheid mto Blood unapita katika kinamasi kikubwa ambayo ni eneo muhimu la kimbilio wakati wa msimu wa baridi kwa ndege wahamao kama bata na bata bukini.[3]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads