Tawimto

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tawimto
Remove ads

Tawimto[1] (kwa Kiingereza: tributary) ni mto unaoishia katika mto mwingine ambao kwa kawaida ni mkubwa zaidi.

Thumb
Mstari buluu mnene ni mto mkuu, mstari mwembamba ni tawimto.

Kwa kawaida maji ya eneo fulani hutiririka chini na kuwa vijito na mito hadi kuishia katika mto mkuu unaobeba maji yote hadi baharini, ziwa kubwa, madimbwi au wakati mwingine katika sehemu ya jangwa yanapopotea. Mto unaofikia mwisho hutazamwa kuwa mto mkuu wa beseni, na mingine yote ni matawimto yake, ama moja kwa moja au kupitia tawimto lingine.

Wataalamu wakiorodhesha mito yote ya beseni la mto fulani hutumia hasa taratibu mbili tofauti za kuorodhesha mito hii:

  • hesabu kutoka chanzo cha mto mkuu kuelekea mdomo
  • hesabu kutoka mdomo wa mto mkuu

Matawimto huorodheshwa kuwa ya kushoto au kulia. Hapo msimamo daima hufuata mwelekeo wa maji kutoka chanzo kwenda mdomoni. Kwa mfano pala ambako mto Ruvuma ni mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji ukielekea Bahari Hindi, mito yote inayoingia Ruvuma kutoka upande wa Msumbiji ni matawimto ya kulia, mito yote inayoingia kutoka upande wa Tanzania ni matawimto ya kushoto.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads