Mto Bushman

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mto Bushmanmap
Remove ads

Mto Bushman (kwa Kiafrikaans: Boesmansrivier) ni mkondo unaotoa maji katika mashariki kwenda kaskazini mashariki mwa mto Tugela, ndani ya KwaZulu-Natal, jimbo la Afrika Kusini.

Ukweli wa haraka Bushman's River, Native name ...
Thumb
Lambo la Mto Bushman.

Mto huo unatoka milima ya Drakensberg, huku eneo lake la juu la kukusanya maji likiwa katika Giant's Castle Game Reserve, mashariki mwa Giant's Castle. Mto huu hupeleka maji yake katika Wagendrift Dam na huendelea kutiririka na kupita katika mji wa Estcourt na hapo huungana na mto Tugela karibu na mji wa Weenen.[1]

Matawimto ya mto huu ni Little Bushmans River ambao huungana na mto Bushman katika Estcourt, Rensburgspruit, mto Mtontwanes na mto Mugwenya. Lambo la Wagendrift karibu na Estcourt ni bwawa kubwa la kuhifadhia maji. Kuna vijiji vingi vyenye idadi kubwa ya watu, vingi vikiwa vinakaliwa na jamii ya amaHlubi, vinapatikana katika eneo la juu la kukusanyia maji.[2] Mto umepakana na Bloukrans River upande wa kaskazini na Mooi River upande wa kusini.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads