Mto Kagera

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mto Kagera
Remove ads

Mto Kagera (kwa Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto Nile, pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.

Thumb
Kagera kwenye maporomoko ya Rusumo. Mto ni mpaka, Tanzania upande wa kushoto na Rwanda upande wa kulia. Vituo vya mpakani vinaonekana darajani.
Thumb
Ramani ya Mto Kagera.

Unaanzia Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela km 400 hadi kuingia ziwa Viktoria.

Mto Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale unapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho ya njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza km kama 40 kaskazini kwa Bukoba.

Jina la mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads