Mtolondo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mtolondo
Remove ads

Mitolondo au bwerenda ni ndege wadogo wa jenasi Lagonosticta katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi lakini madume wana rangi za nyekundu, kahawa na kijivu, pengine pamoja na madoa meupe madogo. Majike wana rangi za kahawa na kijivu kwa kawaida lakini mara nyingi wana sehemu nyekundu pia na madoa meupe kidarini. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi na majani lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-6. Spishi nyingi ni wateswa wa vinili ambao huyataga mayai yao katika matago ya mitolondo.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads