Mwanadiplomasia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mwanadiplomasia (kutoka Kigiriki διπλωμάτης diplōmátēs, yaani mwenye hati rasmi ya kitambulisho) ni mtu aliyeteuliwa rasmi na serikali kuiwakilisha katika nchi nyingine. Taasisi za kimataifa zinazotambuliwa kama vile Umoja wa Mataifa huwa pia na wanadiplomasia.
Kazi
Kazi kuu za mwanadiplomasia ni uwakilishi wa masilahi ya nchi yake pamoja na raia wa nchi inayotuma. Mwanadiplomasia anatekeleza kazi katika jengo la ubalozi wa nchi yake au kama mjumbe wa utume wa kidiplomasia, mara nyingi pia katika Wizara ya Mambo ya Nje kwake nyumbani. Akiwa na cheo cha kuongoza ubalozi.
Haja ya kutambuliwa rasmi
Mkataba wa Vienna juu ya Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961 unaeleza utaratibu unaokubaliwa na nchi zote za Dunia. Mwanadiplomasia anahitaji kibali cha nchi anakotumwa. Nchi anapotumwa inaweza kufuta kibali chake siku yoyote kwa kumtangaza ni "persona non grata", yaani kwamba hatakiwi tena. [1].
Kinga cha kidiplomasia
Ndani ya nchi anakotumwa ana kinga cha kidiplomasia; maana yake hawezi kukamatwa kwa mashitaka, makosa au hata jinai. Anasamehewa kodi na ushuru wote kwa mahitaji yake ya kikazi na ya binafsi.
Sehemu ya kinga hiyo ni hali ya jengo la ubalozi pamoja na nyumba anamoishi balozi kuhesabiwa kuwa "nje ya nchi" (extraterritorial); mtu yeyote pamoja na maafisa wa polisi hawaruhusiwi kuingia bila kibali cha balozi mwenyewe. Kwa hiyo majengo ya kibalozi yalitumiwa wakati mwingine kuhifadhi wakimbizi waliotafutwa na serikali ya nchi yao.
Vyeo
Mwanadiplomasia kiongozi katika nchi fulani kwa kawaida anaitwa "balozi". Akikaimu tu ataitwa "charge d'affaires". Kwa Kiingereza kuna tofauti kati ya "ambassador" na "high commisioner" ambayo ni cheo cha mabalozi kati ya nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth).
Marejeo
Tazama pia
Kusoma zaidi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads