Nabii Yoeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nabii Yoeli (kwa Kiebrania יואל, Yoel, maana yake YHWH ni Mungu) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale, labda katikati ya karne ya 4 KK.

Ujumbe wake unapatikana katika gombo la Manabii Wadogo la Biblia, kwa jina la Kitabu cha Yoeli. Humo tunasoma alivyotangazwa siku tukufu ya Bwana na fumbo la Roho Mtakatifu kumiminwa juu ya kila mtu, ambalo Wakristo wanaamini Mwenyezi Mungu alilitimiza kwa namna ya ajabu katika Yesu Kristo kwenye Pentekoste [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake kwa Wakatoliki na Waorthodoksi huwa tarehe 19 Oktoba[2][3] lakini awali pia tarehe 13 Julai.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads