Mashuke (kundinyota)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mashuke (kundinyota)
Remove ads

Mashuke (pia: Nadhifa) ni kundinyota la zodiaki inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la en:Virgo[1].

Thumb
Nyota za kundinyota Nadhifa (Virgo) katika sehemu yao ya angani
Thumb
Ramani ya Nadhifa - Virgo jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini


Thumb
Uchoraji wa Kiingereza wa karne ya 19 unaonyesha Virgo - Nadhifa akiwa na mashuke (Spica) mkononi

Nyota za Mashuke huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Mashuke" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Remove ads

Jina

Mabaharia Waswahiuli walijua nyota hizi zaidi kwa jina la "Nadhifa" (aliye safi) ambalo ni kifupisho cha Kiarabu العذراء النظيفة al-ʿadhraaʾ an-naḍhiifa yaani "bikira safi". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale. hao walipokea kundinyota hili tayari kutoka Babeli na tangu mwanzo watu waliona uhusianio kati ya nyota hizi na rutba pamoja na miungu wa kike.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Nadhifa" halitumiwi tena ikiwa kundinyota linaitwa "Mashuke" na wakati mwingine pia Sumbula. Ila tu "Sumbula" ni jina la nyota angavu zaidi katika kundinyota hili (Spica, au Alfa Virginis). Asili ya "mashuke/ sumbula" ni picha iliyotumiwa kuchora kundinyota hili iliyokuwa binti anayebeba mashuke ya ngano. Waarabu waliopokea kundinyota pamoja na ishara yake kutoka kwa Wagiriki hawakuchora tena mwili wa binti kutokana na kanuni za dini yao walichora mashuke pekee yanayoitwa "sunbula" kwa Kiarabu. Katika mapokeo ya Kiarabu majina ya "nadhifa" na "sunbula" yalitumiwa sambamba.[2]

Remove ads

Mahali pake

Mashuke iko angani kwenye mstari wa zodiaki kati ya Simba, pia Asadi (Leo) upande wa magharibi na Mizani (Libra) upande wa mashariki.

Magimba ya angani

Kuna nyota nyingi katika eneo la kundinyota hii. Inayoonekana na mashuhuri zaidi ni Sumbula (en:Spica) au "Alfa Virginis". Pamoja na nyota nyingine kuna pia magalaksi kadhaa katika Nadhifa. Nyota zake zimegunduliwa hadi 2017 kuwa na sayari za nje 35 zinazozunguka nyota 29 za Nadhifa.

Maelezo zaidi Jina la (Bayer), Namba ya Flamsteed ...

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads