Sumbula
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sumbula (kwa Kiingereza na Kilatini Spica spi-ka, pia α Alpha Virginia, kifupi Alpha Vir, α Vir) ni jina la nyota angavu zaidi katika kundinyota la Nadhifa (en:Virgo) ikiwa pia nyota angavu ya 15 kwenye anga la usiku.

Jina
Jina la kimataifa ni en:Spica, pamoja na Alpha Virginis[1]. Jina la Kiswahili linatokana na Kiarabu السنبلة al-sunbula[2]. Maneno yote humaanisha "shuke" (mbegu za nafaka) na asili ni unajimu wa Babeli ambako watu waliabudu mungu wa kike wa kilimo waliyemwita shala shubultu yaani Mungu wa Shuke na kumtabua katika nyota akishika shuke mkononi. Kundinyota hili lilipokewa na Wagiriki wa Kale na kutoka huko na Waarabu.
Remove ads
Tabia
Sumbula iko kwa umbali wa miakanuru 250 ± 10 kutoka jua letu. Katika darubini inaonekana si nyota 1 bali nyota mbili zilizo karibu sana na kuzungukana. Kwa sababu hiyo uangavu wa Sumbula unachezacheza kiasi, maana mara tunaona sehemu ya kiangavu zaidi mbele, mara sehemu ya kiangavu kidogo.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads