Simba (kundinyota)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Simba ni kundinyota la zodiaki linalojulikana pia kama Asadi au kwa jina la kimagharibi Leo[1]. Ni moja ya makundinyota yanayotatambuliwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2]



Kiuhalisia nyota za Simba huwa haziko pamoja kama zionekanavyo kutokea duniani. Kuna umbali mkubwa kati ya nyota na nyota, pia kuna umbali mkubwa kati ya mahali zilipo nyota hizo na duniani bila kujali iwapo kwa mtazamo wetu zaonekana kuwa karibu au mbali. Kwahiyo kundinyota "Simba" linaonyesha eneo la angani jinsi lionekanavyo likiangaliwa kutokea duniani.
Remove ads
Jina
Mabaharia Waswahili waliita nyota hizi Asadi kutokana na Kiarabu أسد ʾasad ambalo linamaanisha "simba". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Λέων leon "simba" na hao walipokea kundinyota hii tayari kutoka Babeli na Misri ya Kale. [3] [4]
Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Asadi" limesahauliwa ikiwa kundinyota linaitwa "Simba" kwa tafsiri tu.
Remove ads
Mahali pake
Simba liko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Saratani (Cancer) upande wa magharibi na Nadhifa (Virgo) upande wa mashariki.
Magimba ya angani
Simba huwa na nyota nyingi zinazoonekana kwa macho ya kawaida. Nyota nne angavu zaidi zina magnitudi ya kwanza au pili ambazo ni
- Maliki Junubi[5] (en:Regulus), pia Alfa Leonis ambayo ni nyota nyeupe-bluu yenye uangavu unaonekana wa 1.34, ikiwa na umbali wa miakanuru 77.5 kutoka duniani. Ni nyotamaradufu linayoweza kuonekana kwakutumia darubini ndogo ya mkononi kuwa ni kundinyota lenye nyota mbili zilizokaribiana. Jina lake latokana na Kiarabu ملكى malikiy "kifalme" [6] na جنوبى janubi "kusini"; jina la Kilatini "Regulus" linamaanisha "mfalme mdogo".
- Beta Leonis (en:Denebola) iko upande wa kinyume wa kundinyota na jina la Kimagharibi ni mafupisho ya Kiarabu ذنبالاسد dhanab al asad "Mkia wa Simba". Ina uangavu unaoonekana wa 2.23 ikiwa na umbali wa miakanuru 36 kutoka kwa Dunia.[7]
- Jabuha Asadi[8] (en:Algieba) au Gamma Leonis ni nyota maradufu yenye uangavu unaoonekana wa 2.08 ikiwa na umbali wa miakanuru 126 kutoka dunia. Jina lamaanisha ""paji la uso wa simba".
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads