Nafasi

sifa ya fizikia kwa umbali na mwelekeo From Wikipedia, the free encyclopedia

Nafasi
Remove ads

Nafasi ni mfumo wenye pandeolwa tatu ambao una mahali na mielekeo.[1] Kwa lugha ya kawaida, ni mahali patupu ambapo vitu vinaweza kuwekwa.[2] Katika fizikia kawaida, nafasi mara nyingi hutungwa kama pandeolwa tatu mstari. Wanafizikia wa kisasa kwa kawaida huichukulia, pamoja na wakati, kuwa sehemu ya mfumo wenye pandeolwa nne za nafasiwakati zisizo na kikomo.[3] Dhana ya nafasi ni muhimu kabisa katika kuelewa misingi ya ulimwengu. Hata hivyo, kutokubaliana kunaendelea kati ya wanafalsafa kuhusu kama nafasi ni halisi au sehemu ya mfumo wa dhana tu.

Thumb
Mfumo majiranukta Kartesi mwenye pandeolwa tatu unaotumiwa ili kuonyesha mahali katika nafasi

Katika karne za 19 na 20 wanahisabati walianza kuchungua jiometri ambazo si za Euklides, ambapo nafasi ni kama mchirizo, badala ya kuwa bapa kama katika nafasi ya Euklides. Kwa mujibu wa nadharia ya uhusianifu wa jumla ya Albert Einstein, nafasi karibu na nyuga za uvutano huachana na nafasi ya Euklides.[4] Lakini kwa kiwango kikubwa msongamano wa maada ni takriban sawa kokote ulimwenguni na hivyo ulimwengu ni takriban ya Euklides.[5]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads